You are currently viewing Escobar Babake anyosha maelezo juu ya kusainiwa 001 Music

Escobar Babake anyosha maelezo juu ya kusainiwa 001 Music

Msanii kutoka Pwani Escobah babake amefunguka sababu za kuwa na ukaribu na wasanii wa lebo ya 001 Music.

Kwenye mahojiano yake na Captain Nyota amesema hatua ya yeye kujihusisha sana na wasanii wa lebo hiyo haimaanishi akuwa anajipendekeza kwao ila anafanya hivyo kwa ajili ya kujifunza kuhusu masuala ya tofauti kwenye muziki wao ikizingatiwa kuwa wana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii lakini pia ni wachapa kazi kwenye shughuli zao za muziki.

Kauli ya Escobar Babake imekuja mara baada ya walimwengu kuhoji kuwa anajipendekeza kwa wasanii wa 001 music kwa lengo la kutaka kusainiwa chini lebo hiyo inayomilikiwa na aliyekuwa gavana wa Mombasa Hassan Joho.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke