Ngoma ya Wizkid akiwa amemshiriki Tems, Essence imefanikiwa kufikisha kiwango cha mauzo ya platinum nchini Marekani.
Essence imefanikiwa kuuza jumla ya nakala milioni 1 katika nchini hiyo tangu kuachiwa kwake Oktoba 29, mwaka wa 2020.
Lakini pia wimbo huo ulifikisha mauzo ya Gold Septemba 2, mwaka wa 2021 kwa kuuza jumla ya nakala laki 5 nchini Marekani.
Wimbo wa Essence ambao ni wimbo wa nne kwenye album ya ‘Made In Lagos’ iliyotoka Novemba mwaka wa 2020, unakuwa wimbo wa kwanza kutoka Nigeria kuingia kwenye rekodi hiyo nchini Marekani.