Mke wa msanii Guardian Angel,Esther Musila ametoa changamoto kwa wanawake walio kwenye ndoa kujenga tabia ya kuwaweka waume zao kwenye maombi.
Akipiga stori na SPM BUZZ Musila amesema maombi yana nguvu kubwa sana katika maisha ya ndoa kwa kuwa inaleta familia pamoja lakini pia inawasaidia wanandoa kufanikisha baadhi ya mipango yao.
Mwanamama huyo wa miaka 52 amesema amekoshwa sana na mienendo ya mama taifa Bi Rachel Ruto ya kumtanguliza Mungu kwa kila jambo ambapo amehapa kwamba atafuata nyayo zake kuhakikisha mume wake Guardian Angel anafanikisha ndoto zake katika maisha.
Utakumbuka Guardian Angel na mke wake Esther Musila ni miongoni mwa wasanii watakao toa burudani Septemba 13 katika hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya Dkt. William Samoe Ruto kwenye uga wa kamataifa wa Kasarani.