You are currently viewing EUDOXIE YAO BADO ANA MAPENZI KWA EX WAKE GRAND P, AMTAKIA KHERI KWENYE MAISHA YAKE MAPYA

EUDOXIE YAO BADO ANA MAPENZI KWA EX WAKE GRAND P, AMTAKIA KHERI KWENYE MAISHA YAKE MAPYA

Mwanamitindo mwenye shepu matata kutoka nchini Ivory Coast Eudoxie Yao amemtakia kila la kheri katika maisha aliyekuwa mpenzi wake Grand P, baada ya kumuona kwenye video akijivinjari katika bwawa la kuogelea na mwanamke mwingine.

Katika video hiyo, mwanamuziki huyo kutoka Guinea mwenye umbile dogo zaidi ameposti video Facebook akiwa amejiachia na mrembo wake mpya.

“Maisha ni kitu cha kuvutia sana, jibambe kadri ya uwezo wako. Mimi najivinjari kivyangu,” aliandika Grand P

Katika comment aliyekuwa mpenzi wake, Eudoxie Yao ameandika ujumbe wa kumtakia kila la kheri katika Maisha.

Fununu za kuachana kwa wawili hao zilizuka wakati wa mashindano ya AFCON nchini Cameroon mapema mwezi Februari wakati mwanaume huyo mdogo alipoonekana akiwa na wanawake wengi jambo linalotajwa kumkera Eudoxie na kumpelekea kufanya maamuzi ya kumuacha Grand P.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke