You are currently viewing EUNICE NJERI AWASHANGAZA MASHABIKI KWA KUFUNGA NDOA KWA SIRI

EUNICE NJERI AWASHANGAZA MASHABIKI KWA KUFUNGA NDOA KWA SIRI

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Eunice Njeri ameamua kutupasha tusiyoyajua kuhusu maisha yake ya ndoa baada ya ukimya wa muda mrefu.

Kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya IEBC kutangaza matokeo ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu Njeri ametusanua kuwa alifunga ndoa ya siri mwaka 2021 na mwaka huu amebarikiwa kumpata mtoto wa kiume na mume wake

Hitmaker huyo amesema walichumbiana na mume wake mwaka 2019, wakafunga ndoa mwaka wa 2021 na mwaka 2022 walijaliwa kumpata wa kiume.

“So in other news, I met Mr Muthii in 2019, married him in 2021, and was blessed with a bouncing baby boy in 2022. Glory to God.” Ameandika Instagram.

Utakumbuka Eunice Njeri ambaye anajulikana sana na uimbaji wake wa nyimbo za injili hajawahi weka wazi mahusiano yake ya kimapenzi kwa umma tangu uvumi wa yeye kuikimbia ndoa yake ya kwanza kusambaa sana mitandaoni miaka kadhaa iliyopita.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke