Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Evelyn Wanjiru ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la Mwanga, album ambayo ina jumla ya mikwaju 13 ya moto.
Album hiyo ambayo kwa sasa inapatikana kupitia mtandao wa ku-stream muziki wa Boomplay, haina collabo hata moja, kwani ngoma zote Evelyn kapita nazo mwenyewe.
Album ya “Mwanga” ni album ya nne kwa mtu mzima Everlyn wanjiru tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Celebrate iliyotoka mwaka wa 2019 ikiwa na jumla ya mikwaju 9 ya moto