Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Ray G, Elizabeth Namara amevunja kimya chake baada ya kuonekana akisherehekea kifo cha Binti wa msanii huyo.
Kupitia video ya moja kwa moja iliyoweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, Elizabeth Namara amethibitisha kuwa hajutii kitendo chake cha kufurahia msiba uliomkuta Ray G ambapo amewaonya wanaomkosa waache kufuatilia na masaibu ya mahusiano yake kimapenzi.
“Sitakata tamaa, nataka Ray G ateseke hadi pumzi yake ya mwisho. Nyinyi ambao mnahurumia mnapaswa kukoma kuingilia mambo ya watu zingatieni maisha yenu ya mahusiano. Hamuelewi ni jinsi gan Ray G aliniumiza,” alisema.
Mrembo huyo amesema mwanamuziki huyo atalazimika kumuomba msamaha hadharani ikiwa anataka kuishi maisha ya furaha na familia yake.
Ni kauli ambayo imeibua hisia miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo baadhi wamewashauri Namara asamehe na asonge mbele na maisha yake.
Itakumbukwa Ray G na mkewe, Annabelle, walimpoteza binti yao wa pili ambaye alizaliwa kabla ya wakati wake siku chache zilizopita, jambo ambalo lilimfanya mpenzi wake wa zamani, Elizabeth Namara kufurahia msiba alioupata.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook mrembo huyo alisema kwamba hatatulia hadi pale Ray G atakapolipa uharibifu aliyosababisha katika maisha yake kwa kumpa ahadi za uongo kwamba atafunga ndoa naye.