You are currently viewing EX WEEZDOM, MYLEE STACY ATISHIA KUFUNGULIA MASHTAKA MSANII HYO KWA KUMZUSHIA TUHUMA ZA UONGO

EX WEEZDOM, MYLEE STACY ATISHIA KUFUNGULIA MASHTAKA MSANII HYO KWA KUMZUSHIA TUHUMA ZA UONGO

Mpenzi wa zamani wa msanii Weezdom, Mylee Stacy ametishia kumchukulia hatua kali za kisheria msanii huyo mara baada ya hivi majuzi  kumporomeshea matusi mazito kwa madai ya kuingilia mahusiano yake mapya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mylee Stacy  amepost AOB ikionyesha namna ameandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Ruaka jijini  Nairobi huku akisema kuwa ameamua kufungulia weezdom mashtaka kwa sababu amechoshwa na vituko vyake vya kumvunjia  kila mara kwa kashfa za uongo  ambazo kwa mujibu wake imeshushia brand na kumuathiri kiakili.

Mrembo huyo amekanusha madai yaliyoibuliwa na weezdom kuwa amekuwa akimtumia jumbe za mapenzi na kumpigia simu mke nyakati za usiku kwa kusema kuwa madai hayo ni ya uongo kwani ni njia weezdom kutafuta uhuruma kwa umma.

Hata hivyo mchumba mpya wa Weezdom, Carol Leehavi amekingia kifua msanii huyo a kwa kudai kuwa Mylee Stacy alimsaliti Weezdom kwa kutoka kimapenzi na wanaume mbali mbali jambo ambalo lilipelekea mahusiano yao kuvunjika.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke