You are currently viewing EXRAY AZIMA TETESI ZA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KUPIGWA MARUFUKU

EXRAY AZIMA TETESI ZA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KUPIGWA MARUFUKU

Staa wa muziki nchini Exray amekanusha tetesi zinazosambaa mtandaoni kwamba wimbo wake uitwao Sipapangwi umepigwa marufuku kuchezwa kwenye maeneo ya umma.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Exray amesema madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa ni propaganda zinazosambazwa  na watu wanaotakia mabaya mtandaoni.

Msanii huyo wa kundi la Boondocks gang amewataka mashabiki zake wanaendelea kustream wimbo huo kwenye digital platforms mbali mbali mtandaoni kwani wimbo huo hauna matamshi ya chuki kama inavyodhaniwa.

Utakumbuka wiki kadhaa iliyopita tume ya uwiano na utangamano nchini ilitoa orodha ya maneno yaliyopigwa marufuku kwenye majukwaa ya kisiasa na neno sipangwingwi ilikuwa moja kati ya maneno hayo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke