Msanii wa kundi la Boondocks Gang, Exray Taniua ametunukiwa tuzo ya Silver Play Button na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha jumla ya subscribers laki moja kwenye channel yake.
Exray ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake za muziki huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi.
Channel ya youtube ya Exray ilifunguliwa rasmi Aprili 4 mwaka wa 2017 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 11.3 huku ikiwa na jumla ya subscribers 154, 000.
Utakumbuka tuzo ya Silver Play button huwa inatolewa kwa wanamuziki au watu maarufu kwenye mtandao wa youtube ambao hujizolea zaidi ya subcribers laki moja.