You are currently viewing EZEKIEL MUTU AMKINGIA KIFUA ODINGA KWA KUTUMIA WIMBO WA SAUTI SOL KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA KISIASA

EZEKIEL MUTU AMKINGIA KIFUA ODINGA KWA KUTUMIA WIMBO WA SAUTI SOL KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA KISIASA

Mwenyekiti wa chama cha hakimiliki ya muziki nchini Ezekiel Mutua amefunguka kuhusu utata unaozingira wimbo wa Extravaganza wa kundi la Sauti Sol, uliotumiwa na mrengo wa azimio la umoja kwenye hafla ya kumtambulisha mgombea mwenza wa Raila Odinga.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Mutua amesema azimio la umoja walifuata taritibu zote za kupata leseni ya kutumia wimbo wa extravangaza kwenye kampeini zao.

Mutua ameenda mbali na kudai kuwa amesikitisha namna ambavyo Bodi ya hakimiliki nchini imezua tafrani/hofu miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa kinzani juu kutumika kwa wimbo wa extravagaza ikizingatiwa kuwa jambo hilo lilipaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Hata hivyo amesema katiba ya Kenya imeipa jukumu chama cha hakimiliki ya muziki nchini kukusanya pesa kwa niaba ya wasanii,  hivyo hakuna namna ambavyo watakwenda kinyume na sheria za hakimiliki.

Hata hivyo msanii wa Sauti Sol, Bien amesema hawatalegeza msimamo wao wa kuichukulia hatua  kali za kisheria timu ya raila odinga kwa kukiuka hakimiliki ya bendi hiyo licha ya watu kuwabeza kwenye mitandao ya kijamii.

Utakumbuka Mei 17 mwaka huu Raila Odinga alidai kuwa walitumia wimbo huo kama njia ya kuionesha upendo kundi la Sauti Sol ambalo limeipeperusha bendera ya Kenya kimataifa

 

 

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke