You are currently viewing FACEBOOK YAANZA KUWEKA REELS KATIKA APP YAKE

FACEBOOK YAANZA KUWEKA REELS KATIKA APP YAKE

Facebook iliweka videos fupi katika mtandao wa Instagram zilizopewa jina la Reels, mbinu ambayo inasemekana ni kushindana na soko la TikTok na YouTube Shorts kwa sababu imeonekana kuna watu wengi wanapendelea short videos.
 
Sasa habari njema ni kwamba Facebook imeanza kuweka rasmi Reels katika app yake ya Facebook kwa watumiaji wa Marekani na imesema itaweka katika nchi zote zilizobaki. Watumiaji wa Facebook wataweza kuweka Reels na kushare katika mtandao wa Instagram na Facebook.
 
Reels za Instagram pia zitaweza kuonekana katika mtandao wa Facebook na mpangilio na muonekano unaonekana kama Instagram Reels na TikTok. Reels za Facebook zitakuwa na Audio, AR Effects, Timer/Countdown/Speeds na sehemu ya Multi Clips ambayo itawezesha watumiaji kumix videos.
 
Watumiaji wa Facebook wataona tab mpya ya “Reels” katika app ya Facebook na hivi karibuni itaanza kupatikana kwa watumiaji wa nchi zote duni kwani ni update ambayo imeanza rasmi leo.
 
 
 
 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke