You are currently viewing FAMILIA YA KIJANA ALIYEUWAWA NYUMBANI KWA SPICE DIANA YATAKA HAKI

FAMILIA YA KIJANA ALIYEUWAWA NYUMBANI KWA SPICE DIANA YATAKA HAKI

Familia ya Henry Nsamba kijana anayedaiwa kupigwa nyumbani kwa Spice Diana na baadae akafariki Hospitalini inashinikiza kukamatwa kwa mwanamuziki huyo kutoka Uganda.

Inadaiwa kuwa mwendazake ambaye alikuwa mfanyikazi wa kutengeneza matofali alifumaniwa Juni 30 mwaka huu akitaka kutekeleza kitendo cha wizi wa nyumbani kwa Spice Diana ndiposa akashushiwa kichapo cha mbwa kilichompelekea kufariki.

Johnson Matovu,  ambaye ni baba mzazi wa mwaasiriwa ameeleza kuwa alionana na kijana wake huyo siku kadhaa zilizopita lakini alipatwa na mshtuko alipopokea taarifa za kifo chake kwa njia ya simu.

Matovu amesema alitofautiana kimawazo na mwanae Nsamba alipotaka kujiunga na muziki jambo ambalo lilimfanya mwanae huyo kukimbia nyumbani na kwenda kutafuta maisha kivyake.

Hata hivyo amewataka vyombo vya usalama viharakishe uchunguzi wa kubaini kifo cha mwane Henry Nsamba huku akitoa wito kwa washukiwa wakuu akiwemo Spice diana kukamatwa.

Mapema wiki hii Spice Diana alitarajiwa kuhojiwa katika makao makuu ya idara ya upelezi DCI kuhusu tuhuma za mauji yanayomkabili kwa lakini msanii huyo alisusia na kuzima simu zake zote.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke