Familia ya mwanamuziki mkongwe nchini Kenya, Patonee imekubali achangiwe fedha za matibabu wakati huu anaendelea kuhudumiwa hospitalini.
Kulingana familia ya msanii huyo, patonee ambaye alikimbizwa hostipali Oktoba mosi mwaka huu yupo kwenye hali mbaya katika katika chumba cha uangalizi maalumu wa wagonjwa (ICU) ambapo gharama ya matibabu yake inazidi kuongezeka kadri siku zinaposonga mbele.
Hata hivyo wamewaomba wahisani kujitokeza na kuwasaidia kuchangisha pesa za kugharamia matibabu ya msanii huyo kupitia M-Changa: Patrick Mwangi – [Paybill Number: 891300], [Account Number: 58759].
Tayari wasanii na mastaa mbalimbali nchini Kenya wameweka tangazo hilo kama njia ya kuunga mkono kupatikana kwa mchango huo akiwemo Big Pin.
Utakumbuka Patonee alipata umaarufu kupitia wimbo uitwao Talk 2 you aliomshirikisha Big Pin na Amani mwaka wa 2004 na tangu kipindi hicho alipotea kwenye tasnia ya muziki na kuwaacha mashabiki wakiwa na kiu ya muziki wake.