Rapa wa kike nchini Femi One ameamua kurudisha fadhila kwa uongozi wake wa Kaka Empire ambao umemtoa kimuziki hadi kujulikana Afrika Mashariki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Femi One ametoa ametoa shukrani zake za dhati kwa mabosi wake King Kaka na Dennis Njenga kwa kumsaidia kufika alipo leo kwenye muziki ambapo ameenda mbali zaidi na kujitolea kuwanunulia wawili hao magari kama njia ya kuzawadi kwa kumshika mkono kisanaa.
“Mapenzi na heshima nyingi sana kwa waungwana hawa wawili. Nikikumbuka safari yetu ya muziki huwa natabasamu tu ila wakati mwingine huwa nalia š Moyo wangu umejaa shukrani nyingi King Kaka na Dennis Njenga ingieni showroom mchague magari mnayotaka!”
Femi One alijiunga na lebo ya muziki ya Kaka Empire mwaka wa 2013 baada ya kuonesha uwezo wake kisanaa kupitia wimbo wa Ligi Soo Remix wake rapa King Kaka na tangu kipindi hicho amekuwa akiachia nyimbo kali mfululizo bila kupoa.
Kando na muziki, Femi One pia mwaka 2021 aliandika historia ya kuwa Balozi wa Kwanza wa Kike kutoka barani Afrika wa Kinywaji cha Monster Energy.