Rapa Femi One ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo huenda akamshirikisha Nyashinsiki au Khaligraph Jones.
Kwenye mahojiano na The Trend ya NTV rapa huyo ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Lip Service” amesema yupo mbioni kufanikisha hilo kwa kuwa tayari ameanza mazungumzo na marapa hao kuhusu mpango wa kufanya EP ya pamoja.
Utakumbuka Femi One amefanya kazi ya pamoja na Nyashinski kupitia wimbo uitwao “Properly” na Khaligraph Jones kupitia ngoma inayokwenda kwa jina la “Blue Ticks”.