Rapa kutoka Kenya, Femi One anaendelea kupokea upendo na support kubwa kutoka kwa mashabiki wake kiasi cha kufanya vizuri kwenye mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa BoomPlay.
Hadi kufikia sasa katika mtandao wa Boomplay Kenya Femi One amefanikiwa kufikisha zaidi ya streams Million 5 kupitia nyimbo zake zote.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Femi One amewashukuru mashabiki zake kwa support wanayompa kila siku huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani na ngoma kali zaidi.
Ikumbukwe Album ya “Greatness” ambayo ndio albamu ya kwanza kwa femi one tangu aanze muziki wake imefanikiwa pia kufikisha zaidi ya Streams millioni 1.2 kwenye mtandao wa Boomplay.
Album ya Greatness iliachiwa rasmi mwezi Juni, 2 mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 14 ya moto huku ikiwa na kolabo 9 pekee.