Fifa inachunguza jinsi mpishi maarufu Salt Bae na watu wengine kadhaa walipata “nafasi isiofaa” kufika uwanjani mwishoni mwa fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar.
Salt Bae, mpishi wa Uturuki ambaye jina lake halisi ni Nusret Gokce, alionekana katika picha akiwa ameshika na kubusu kombe la Kombe la Dunia akisherehekea na wachezaji wa Argentina baada ya ushindi wao dhidi ya Ufaransa.
Sheria za Fifa zinasema kombe hilo linaweza tu kushikiliwa na kundi la watu “walioidhinishwa”, wakiwemo washindi wa mashindano, maafisa wa Fifa na wakuu wa nchi.