You are currently viewing FIK FAMEICA ADOKEZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

FIK FAMEICA ADOKEZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

Mwanamuziki kutoka Uganda Fik Fameica ameweka wazi tarehe ambayo tamasha lake la muziki litakalofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Fameica amesema tamasha lake liitwalo ” Fik Fameica live in concert” litafanyika Agosti 26 mwaka huu katika hoteli ya Africana jijini Kampala.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Kanzunzu”  licha ya kutoweka wazi kiingilio na wasanii watakaomsindikiza kwenye tamasha lake la muziki, amesema ataendelea kutoa taarifa zaidi kwa mashabiki zake kwenye mitandao yake ya kijamii.

Hii sio mara ya kwanza kwa Fik Fameica kuandaa tamasha lake mwenyewe mwaka wa 2018 alifanya tamasha liitwalo “My Journey” huko Cricket Oval Lugogo nchini Uganda ingawa haikupata mapokezi mazuri

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke