You are currently viewing FIK FAMEICA ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA AFRIKA MASHARIKI KUJA NA SOUND YA MUZIKI WAO

FIK FAMEICA ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA AFRIKA MASHARIKI KUJA NA SOUND YA MUZIKI WAO

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Fik Fameica ametoa wito kwa wasaniii kutoka Uganda, Kenya na Tanzania kuungana kwa ajili ya kuja na sound itakayotambulisha muziki wa Afrika Mashariki kimataifa.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Fik Fameica amesema muziki wa Nigeria uitwao Afro-Beat umeufunika muziki wa Afrika mashariki kuweza kutambulika duniani kutokana ukanda huu kukosa jina linalowakilisha muziki wake.

Hata hivyo Hitmaker huyo wa ngoma ya “Property” ametoa changamoto kwa wasanii wa Afrika Mashariki kuja na jina litakalotenganisha muziki wao na wa mataifa mengine ya Afrika kama ilivyo kwa muziki wa Amapiano kutoka Afrika kusini.

Fik Fameica anaungana na mtu mzima Harmonize ambaye amekuwa moja kati ya wasanii ambao wamekuwa wakishinikiza muziki wa Afrika Mashariki uwe na jina moja kama ilivyo kwa muziki wa nigeria na Afrika kusini.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke