You are currently viewing FIK FAMEICA AWATOLEA UVIVU WASANII WA UGANDA, ACHANENI WIVU PIGENI KAZI

FIK FAMEICA AWATOLEA UVIVU WASANII WA UGANDA, ACHANENI WIVU PIGENI KAZI

Msanii  wa muziki kutoka uganda Fik Fameica amewatolea uvivu wasanii wa uganda wanaopiga vita wasanii wa nigeria kwenye tasnia ya muziki nchini humo.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Hitmaker huyo wa Kanzunzu amewataka wasanii wa uganda kuacha kasumba ya kuwachukia wasanii wa nigeria na badala yake wajifunze kutoka kwao namna ya kufanikiwa kimuziki kwani ni wasanii ambao wanafanya vizuri duniani.

Fameica ambaye alipata shavu ya kufanya kazi na kampuni ya empewa africa inayomilikiwa na Mr. Eazi ametoa changamoto kwa wasanii wa uganda kuwekeza kwenye muziki wao badala ya kutoa muziki usiokidhi viwango vya kimataifa

“Nigerian music is popular worldwide. Those guys have done well. Instead of fighting them, we should embrace and learn from them,” amesema Fameika.

Utakumbuka Wasanii wengi nchini Uganda wamekuwa wakiwalaumu mapromota wa muziki kwa kuwazingatia sana wasanii wa nigeria kwenye shoo zao huku wakiwatenga wasanii wa ndani jambo ambalo walihoji kuwa ni njia ya kuua muziki wao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke