Mwanamuziki wa kike kutoka nchini Uganda Fille Mutoni ametangaza kuachia EP mpya ndani ya mwaka wa 2022 baada ya kimya cha muda mrefu.
Fille amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea EP yake mpya ambayo kwa mujibu wake itakuwa na jumla ya nyimbo 6 za moto.
Fille ambaye anafanya poa na ngoma yake mpya iitwayo “Oli Wange” alikuwa kimya kwenye muziki wake kwa muda baada ya kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya lakini kwa sasa ametangaza kuja na ujio mpya kwa ajili ya kuwapa mashabiki zake ladha tofauti ya kazi zake walizokuwa wamekosa kutoka kwake.