You are currently viewing FIREBOY DML KUTOKA NIGERIA KUTUMBUIZA KWENYE TUZO ZA BET

FIREBOY DML KUTOKA NIGERIA KUTUMBUIZA KWENYE TUZO ZA BET

Mwanamuziki nyota wa muziki kutoka Nigeria FireBoy ametajwa atatumbuiza kwenye hafla ya kugawa Tuzo za BET mwaka huu ambazo zitafanyika  Juni 26 katika ukumbi wa Microsoft Theater, Jijini Los Angeles.

Tuzo hizo ambazo huandaliwa na Black Entertainment Television (BET) tangu Juni 19, mwaka 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo.

FireBoy anakuwa msanii pekee toka Afrika kutumbuiza siku hiyo, ambapo ataungana na wasanii wengine kutoka Marekani kama Roddy Ricch, Chance The Rapper, Jack Harlow, Lizzo, Joey Bada$$, Latto, na Chlöe.

Kando na hilo, mwaka huu tuzo hizo zitashereheshwa na mwigizaji Taraji P. Henson ikiwa ni kwa mwaka wa pili mfululizo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke