Msanii wa Bongo Fleva, Frank Fredrick maarufu kama Foby,ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Me Myself and I.
Me Myself and I EP ina jumla ya ngoma 5 ambazo amezifanya kama msanii wa kujitegemea.
Ep hiyo ina ngoma kama Joto, Muda, Put It Down,Nitamsea wapi na inapatikana kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mitandaoni.
Me Myself and I ambayo ni Ep ya pili kwa mtu mzima Foby inatoka siku chache tangu atoe ombi kwa wasanii wenzake wasitoe EP zao katika kipindi cha siku 10.
Mkali huyo wa ngoma ya “Kutamu” alitoa ombi hilo la siku 10, yaani kuanzia Desemba 2 hadi 12 mwaka huu.