You are currently viewing FOBY AANDIKA BARUA YA WAZI KWA WADAU WA MUZIKI WA BONGOFLEVA

FOBY AANDIKA BARUA YA WAZI KWA WADAU WA MUZIKI WA BONGOFLEVA

Mwanamuziki na mwandishi wa muziki kutoka Tanzania, msanii Foby ameandika barua ya wazi kwa mashabiki wa Bongofleva, Basata na Tuma (Chama cha Muziki wa Kizazi kipya) kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuachia wimbo wake mpya kabla ya mwezi huu kuisha.

Kwenye barua hiyo aliyoposti kupitia ukurasa wake wa instagram, Foby ameeleza kwamba mara zote amekuwa akitoa nyimbo kali zenye kuelimisha jamii na kutumia tafsida ila kwenye wimbo wake huu mpya ameomba kusamehewa kwani na yeye anataka hela.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ode” amebainisha kuwa ana nyumba yake anataka kuimalizia.

Foby kwenye maelezo yake ya mwishoni katika barua hiyo ametaka majibu ya alichokieleza na endapo yatachelewa amedai kuachia wimbo huo hata leo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke