You are currently viewing FOBY AUPONDA UWEZO WA MARIOO KWENYE MUZIKI WA BONGOFLEVA

FOBY AUPONDA UWEZO WA MARIOO KWENYE MUZIKI WA BONGOFLEVA

Msanii wa Bongofleva Foby amefunguka kuwa mkali wa ngoma ya “Beer tamu” Marioo hawezi kuvikwa taji la Ufalme wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, mwanamuziki huyo amedai kwamba Marioo hawezi kuwa mfalme wa muziki wa Bongofleva ikiwa anaimba muziki wa Amapiano, kwani mfalme anatakiwa kukuza na kufanya mziki wao wa nyumbani na sio kuiga muziki kutoka mataifa mengine.

HitMaker wa ngoma ya “Ode” amechukizwa na kitendo cha rapa Damian Sol kumkana hadharani kwamba hamfahamu kwa kusema kuwa rapa huyo amewavunjia heshima vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikipiga nyimbo zake ikizingatiwa kuwa wamekutana mara nyingi kwenye matamasha mbali mbali ya muziki.

Ikumbukwe Foby kwa sasa anafanya vizuri kwenye Digital Platforms mbali mbali na EP yake iitwayo ME, MYSELF & 1 ambayo aliiachia rasmi mwishoni mwa mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 5 ya moto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke