You are currently viewing FRANK LAMPARD MBIONI KUKINOA KIKOSI CHA LEICESTER CITY

FRANK LAMPARD MBIONI KUKINOA KIKOSI CHA LEICESTER CITY

Kocha wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard, anaamini amekaa nje ya kazi kwa muda mrefu, hivyo yuko tayari kurudi kabla ya msimu huu kufikia ukomo.

Lampard mwenye umri wa miaka 43, ambaye aliinoa Chelsea kwa miezi 10 kabla ya kufukuzwa, alikuwa akihusishwa na Crystal Palace, Newcastle na Norwich City, kabla ya timu zote hizo kupata makocha.

Kwa mujibu wa taarifa, huenda safari hii akaibukia kwenye benchi la ufundi la Leicester City kwa kuwa mabosi wa timu hiyo wanahisi kocha wao, Brendan Rodgers, ataondoka.

Hofu ya Leicester kumpoteza Rodgers inakuja baada ya Manchester United kutajwa kuitaka huduma ya kocha huyo ili akakalie kiti cha Ole Gunnar Solskjaer anayeonekana kushindwa kuhimili ushindani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke