You are currently viewing FRENCH MONTANA AFUNGULIWA KESI KWA TUHUMA ZA WIZI WA WIMBO

FRENCH MONTANA AFUNGULIWA KESI KWA TUHUMA ZA WIZI WA WIMBO

Rapa kutoka marekani French Montana ameburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kuiba mistari ya wimbo wa kundi maarufu la Hip Hop “Hot Boys” lililovuma miaka ya 90.

Rapa Turk ambaye ni memba wa kundi hilo amesema Montana ametumia mistari kwenye wimbo wake mpya “Hand stand” kutoka kwenye wimbo wao wa mwaka wa 1999  uitwao “I Need A Hot Girl”.

Turk anadai French Montana anaingiza pesa kupitia wimbo wake huo ambao tayari una zaidi ya views milioni 17 kwenye mtandao wa YouTube.

Utakumbuka Kundi la “Hot Boys”  liliundwa na wakali kama Lil Wayne, B.G na Juvenile.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke