You are currently viewing FUTURE AUZA HAKI ZA NYIMBO ZAKE KWA KAMPUNI YA INFLUENCE MEDIA PARTNERS

FUTURE AUZA HAKI ZA NYIMBO ZAKE KWA KAMPUNI YA INFLUENCE MEDIA PARTNERS

Rapa kutoka Marekani Future ameripotiwa kuuza haki za nyimbo zake za kuanzia mwaka 2004 hadi 2020 kwa kampuni ya Influence Media Partners.

Tovuti za Variety na Billboard zimeripoti, dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya kuanzia millioni 7 hadi 9 za Kenya.

Catalog iliyouzwa na Future ina jumla ya nyimbo 612 ikiwemo kolabo za wakali kama Drake, Kendrick Lamar, Rihanna na The Weeknd.

Mwaka 2022 kampuni ya Influence Media Partners ilitumia kiasi cha billioni 36 kununua haki za nyimbo za Bruno Mars, Dua Lipa, Ariana Grande na Justin Bieber.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke