Mwanamuziki wa Bongofleva Gnako anauanza mwaka 2023 kwa burudani kali kwa mashabiki wake.
Mkali huyo kutoka Weusi Kampuni ametangaza kuachia Extended Playlist (EP) yake mpya Februari 3, iitwayo Make You Dance.
EP hiyo na ina jumla ya ngoma 7 pekee ambazo ni Mtoto wa mtu, Tusipangiane, How you move, Energy, Macho acha shobo, Hiyo hapo na Tocome.
Gnako amewashirikisha wanamuziki kama Rayvanny, Femi_one Young Daresalama na wenginne wengi.