You are currently viewing G NAKO AWABARIKI MASHABIKI NA KITIMOTO MINITAPE

G NAKO AWABARIKI MASHABIKI NA KITIMOTO MINITAPE

G-nako ni kati ya ma rappers wanaojua nini cha kuwapa mashabiki wao na kwa muda gani! Rapper huyo ambaye ni moja ya wanoaunda kundi la Weusi mara zote huwa hafanyi kazi mbovu, iwe ni ya kwake au ameshirikishwa.

Kwa kujali mashabiki wake kuelekea mwishoni mwa mwaka 2021, G-Nako ameachia Minitape ambayo ameipa jina la ‘Kitimoto’ Watu wengi wanaweza kushangaa jina la Minitape hii, lakini kimsingi G-Nako mwenyewe amemaanisha Kiti chenye Moto yaani mtu huwezi kukaa kwenye kitu muda wote lazima usimame kutokana na ukali wa ngoma zilizopo kwenye Minitape hii kwani zote ni ‘Club Banger.

Minitape hii ya G Nako inajumuisha jumla ya ngoma 9 za moto zenye kolabo za wasanii mahiri wenye sifa ya kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania akiwemo Young Lunya, Country Wizzy na Petra.

Huu unakua ujio wake mpya baada ya miezi tisa kupita bila ya kuachia kazi zake mwenyewe kama solo artist tangu aachie wimbo wake wa mwisho ambao ni “Jiachie” uliotoka Machi 4, 2021.

Minitape hii kwa sasa inapatikana kwenye mtandao namba moja barani Afrika wa kusambaza muziki duniani kote ‘Boomplay

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke