Msanii wa muziki kutoka Kenya Gabiro Mtu Necessary ametangaza kuachia album yake mpya inayokwenda kwa jina la Saint Joint mwishoni mwa wiki hii.
Gabiro Mtu Necesary ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwawataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea album hiyo ambayo kwa mujibu wake ipo itaingia sokoni Aprili 29 mwaka huu.
Licha ya kutoweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album yake mpya, Hitmaker huyo wa ngoma ya “Okay” ametoa wito kwa mashabiki ku-pre-order Saint John album kupitia wavuti wake wa www.gabiromtunecessary.com
Saint Joint Itakuwa Album Ya Kwanza kwa Gabiro Mtu Necesary ,ikizingatiwa kuwa Tayari ana Ep Mbili Alizoachia mwaka mwaka wa 2020 na 2021 mtawalia ambazo ni Jenesis, na Mpito.
Utakumbuka mwaka wa 2021 alipata umaaarufu nchini baada ya ep yake iitwayo Jenesis kuingia kwenye hatua ya kujadiliwa yaani Consideration kwa ajili ya kuingia kuwania Tuzo za Grammy.