Msanii Geosteady ni moja kati ya wanamuziki wazuri wa Rnb kutoka Uganda.
Kwa miaka mingi amekonga nyonyo za wapenzi wa mziki mzuri afrika mashariki na nyimbo kama Same way woman na nyingine nyingi.
Onesho lake la kila mwaka liitwalo Dine with Geosteady ambalo lilifanya vizuri kipindi cha nyuma nchini Uganda ilisimamishwa na ujio wa janga la corona.
Baada ya uchumi kufunguliwa nchini humo.wengi walidhani geosteady atatangaza tarehe ya kufanyika kwa onesho lake kama namna wasanii wengi wanavyofanya.
Lakini bosi huyo Blackman Records hajaonyesha nia ya kufanya hivyo kwani amedai kuwa hana nyimbo za kutosha kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki zake.
“Ziko tayari kwa ajili ya onesho la muziki. Sina muziki wa kutosha”, Geosteady amesema kwenye mahojiano na Galaxy FM.
Utakumbuka miongoni mwa wasanii ambao wanapanga kufanya matamasha yao ya muziki nchini uganda ni pamoja na Levixone, Chameleone, Azawi na wengine wengi.