Msanii kutoka nchini Uganda Geosteady amekanusha kurudiana na baby mama wake Prima Kardash kufuatia uvumi unaosamba mtandaoni kuwa wawili hao wanatoka kimapenzi.
Kwenye mahojiano na karibuni yake amesema ukaribu wao ulikuwa ni kwa ajili ya kuitangaza show yake itakayofanyika leo aliyoipa jina “Dine With Geosteady”
“Alionekana tu kwa video yangu. Hakuna kitu kingine zaidi ya hiyo. Tuna ukaribu kwa sasababu ananisaidia kutangaza show yangu. Sisi sio wapenzi”, Alisema.
Geosteady na Prima Kardashi ambao wana watoto watatu kwa pamoja walivunja mahusiano yao miaka mitatu iliyopita na kila mmoja akaingia kwenye mahusiano mengine.
Prima alikuwa kwenye mahusiano na Mr.Henrie lakini wakavunja mahusiano yao huku Geosteady akianzisha mahusiano na mrembo aitwayo Hindu kisha baadae akahamia kwa Minaj ambaye wamezaa mtoto mmoja.