You are currently viewing GEOSTEADY: “SIJAONANA NA WANANGU KWA MIAKA MITATU SASA”

GEOSTEADY: “SIJAONANA NA WANANGU KWA MIAKA MITATU SASA”

Staa wa muziki nchini uganda Geosteady amefunguka kwamba ana miaka mitatu sasa hajawatia machoni watoto wake ambao alizaa na Baby mama wake Prima Kardash.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Geosteady amesema baby mama wake Prima amekuwa kizingiti kwake kuwaona watoto wake ikizingitiwa  kuwa mara ya mwisho kuwaona ilikuwa mwaka wa 2022.

Hitmaker huyo wa “Energy” anasema anaamini siku moja atakuja kuonana na watoto wake ila kwa sasa amehamua kuelekeza nguvu zake kwenye muziki wake ambao kwa mujibu wake utamuingiza kipato kizuri ambayo itamsaidia kuwalea watoto wake hao siku za usoni.

Wawili hao waliachana miaka mitatu iliyopita wakiwa wamejaliwa watoto wawili na kila mmoja kwa sasa amesonga mbele na maisha yake kwa kuingia kwenye mahusiano mapya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke