You are currently viewing GIGY MONEY ADAI ALIKIBA ANATUMIA BIFU YAKE NA DIAMOND PLATINUMZ KUINGIZA KIPATO

GIGY MONEY ADAI ALIKIBA ANATUMIA BIFU YAKE NA DIAMOND PLATINUMZ KUINGIZA KIPATO

Msanii wa Bongofleva, Gigy Money amedai kuwa Alikiba ananufaika zaidi na bifu yake na Diamond Platnumz. 

Akizungumza na Wanahabari jana katika hafla ya uzinduzi wa WasafiBet, Gigy amedai hilo ndio linafanya hawapatani kwani wote kuna namna wananufaika.

“Alikiba ananufaika zaidi na bifu na Diamond, unataka kukataa?, wapatane basi, kwani shida ni nini?, kuna mtu kamuulia mtu pale? ndio ujue” amesema Gigy na kuendelea; 

“Sio Simba na Yanga wale, ni wanamuziki tu ambao sisi tunawapenda, tunawaheshimu na tunawasapoti kazi zao ila wenyewe hawasapotini kwa sababu wananufuika na lile bifu lao.” amesema Gigy Money.

Ikumbukwe juzi kati Alikiba alipotua nchini aliulizwa na Wanahabari kama naye anaweza kufungua kampuni ya Bet na kujibu hawezi kutokana na dini yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke