You are currently viewing GIGY MONEY ADAI HARMONIZE SIO MSANII MKUBWA KWAKE

GIGY MONEY ADAI HARMONIZE SIO MSANII MKUBWA KWAKE

Video vixen kutoka nchini Tanzania ambaye anatambulika kama msanii kwa sasa Gigy Money amedai kuwa msanii Harmonize si msanii mkubwa kwake bali amemzidi na kumpita mafanikio tu.

Gigy Money amefunguka hayo akijibu swali kuhusu kufanya kazi na mwanamuziki huyo kutoka KondeGang katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, kwa kudai kuwa mtu hawezi badilisha mtazamo wake, kwani anajua msanii huyo kabla hata hajaanza muziki kutoka record label ya WcB, hivyo ni msanii aliyempita kwa mafanikio lakini si mkubwa kwake.

Aidha mwanadada huyo ameongeza kuwa bado hajafikiria kufanya kazi yoyote na msanii huyo kwani anamuona ni msanii wa kawaida kwake

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke