You are currently viewing GILAD MILLO APATA URAIA WA KENYA

GILAD MILLO APATA URAIA WA KENYA

Hitmaker wa Sema Milele, Msanii wa Gilad Millo hatimaye amepata uraia wa Kenya baada ya miaka 21.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Millo ameshindwa kuficha furaha yake kwa kushare Cheti chake cha kusajiliwa kama Raia wa Kenya, ambapo amedokeza kwamba alituma ombi la kutaka Uraia huo miaka 6 iliyopita.

Msanii huyo amesema alikuja Nairobi mara ya kwanza nchini mwezi Agosti mwaka wa 1996 kama mwanafunzi wa chuo kikuu baada ya kuchukua likizo ya mwezi moja na mpenzi wake lakini baadae alirejea nchini mwaka wa 2002.

Gilad Millo ambaye alifanya kazi kama mwanahabari, alikuwa mwanadiplomasia mwaka wa 2003 akihudumu Nairobi na Los Angeles nchini marekani kabla ya kuacha wizara ya mambo ya nje ya Israel mwaka wa 2008 ambako aliamua kuishi jijini Nairobi kabisa.

Ikumbukwe Gilad millo alianza safari yake ya muziki mwaka wa 2015 alipoachia singo iitwayo Unajua akiwa amemshirikisha wendy kimani na mpaka sasa ana album moja ya muziki inayokwenda kwa jina la Asante.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke