You are currently viewing GLORIA MULIRO AFUNGA NDOA NA PASTA EVANS SABWAMI.

GLORIA MULIRO AFUNGA NDOA NA PASTA EVANS SABWAMI.

Msanii wa nyimbo za injili nchini Gloria  Muliro amefunga  rasmi ndoa na mchumba wake wa siku nyingi Evans Sabwami kwenye hafla ya siri iliyohudhuriwa na wanafamilia huko New York chini Marekani.

Hii imekuja wiki chache zilizopita baada ya kumvisha pete mchumba wake Evans Sabwami ambapo walienda mbali zaidi na kufunga ndoa ya kitamaduni maarufu kama ruracio mjini Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu.

Gloria Muliro ameshare picha ya harusi yao kwenye ukurasa wa instagram na kuweka wazi kuwa wao ni mke na mume.

Picha hizo za Gloria Muliro na mpenzi wake Evans Sabwami imeibua hisia za mashabiki wake na mastaa wenzake ambao wameenda mbali na kumpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo kubwa maishani.

Hii ni ndoa ya pili kwa Gloria Muliro, awali alikuwa kwenye ndoa  na pastor eric ambapo walidumu kwenye ndoa kwa takriban miaka sita lakini walikuja wakaaachana rasmi mwaka wa 2015 baada ya ndoa yao kuingiwa na ukungu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke