Mwanamuziki nyota kutoka nchini Guinea Moussa Sandiana Kaba maarufu kama Grand P , ameamua kuchora tattoo yake ya kwanza katika mwili wake kwa kuandika jina la mpenzi wake mwenye umbo kubwa kumzidi, Eudoxie Yao.
Grand P amechora tattoo inayosomeka ‘ ππππ πππ ππππ ‘ akionesha ni kwa namna gani anampenda mpenzi wake huyo raia wa Ivory Coast.
Wawili hao walioata umaarufu zaidi mitandaonI kutokana na muonekano wa maumbo yao, ambapo Grand P yeye akiwa na ugonjwa wa kudumaa na kuonekana kuwa nA umbo dogo, huku mpenzi wake Eudoxie Yao akiwa na umbo kubwa kumzidi.
Haya yanajiri ikiwa ni takribani miezi miwili kupita baada yaΒ GrandΒ PΒ kumvisha Eudoxie pete ya uchumba.