You are currently viewing GRAND P AMVISHA PETE MPENZI WAKE EUDOXIE YAO

GRAND P AMVISHA PETE MPENZI WAKE EUDOXIE YAO

Mwanamuziki kutoka nchini Guinea, ‘Grand P’ amemvisha pete mpenzi wake wa muda mrefu Eudoxie Yao ambaye ni raia wa Ivory Coast.

Wapenzi hao wawili walikuwa kwenye mahojiano na moja ya runinga nchini Gabon ambapo Grand P alipiga magoti na kumvisha Eudoxie Pete na kuahidi kutorudia makosa yaliyosababisha uhasama kati yao awali.

Haya yanajiri ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu wawili hao watengane kutokana na tetesi za Eudoxie kwamba Grand P hakuwa mwaminifu.

Mrembo Eudoxie Yao alitangaza kuachana na Grand P, Julai mwaka 2021 baada ya picha za Grand P akimbusu mwanamke mwingine kusambaa mitandaoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke