Mwanamuziki mwenye umbo dogo kutoka nchini Guinea Grand P ameteuliwa kuwa balozi wa utamaduni na utalii kuliwakilisha taifa hilo kwenye nchi jirani ya Mali
Grand P kupitia ukurasa wake wa Facebook amemshukuru Kanali Mamadi Doumbuya ambaye anashikilia wadhfa wa Urais wa mpito nchini Guinea kwa kumpatia pasipoti ya kidiplomasia huku akisisitiza dhamira yake ya kufanya kazi kwa ajili ya kukuza Utamaduni wa Guinea kama kivutio cha watalii.
Grand P ambaye alizaliwa mwaka 1990 huko Sanguiana, nchini Guinea, amekuwa gumzo mtandaoni kutokana na watu kuzungumzia maumbile yake yasiyo ya kawaida na gumzo hilo lilizidishwa hata zaidi baada ya kuweka wazi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo kutoka Ivory Coast, Eudoxie Yao ambaye ni mkubwa zaidi kwa muonekano wa mwili.