You are currently viewing Gravity Omutujju aandika Cricket Oval, Lugogo kupitia tamasha la Tusimbudde

Gravity Omutujju aandika Cricket Oval, Lugogo kupitia tamasha la Tusimbudde

Rapa kutoka Uganda Gravity Omutujju ameshindwa kuficha furaha yake baada ya watu zaidi ya 30, 000 kujaza ukumbi wa Cricket Oval Lugogo usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha lake la muziki llitwalo “Tusimbudde”

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa “Enyama” amemshukuru mwenyezi Mungu na mashabiki zake kwa kumuonyesha upendo kipindi ambacho walimwengu walikuwa wanasubiri anguko lake kwenye muziki.

Utakumbuka mwaka 2017 Omutujju alijaza nyomi la mashabiki katika ukumbi wa Cricket Oval Lugogo huko Jijini Kampala ambako alipiga show ya kufa mtu iliyowaacha mashabiki wakiwa na kiu ya kutaka burudani zaidi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke