Rapa kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram omutujju ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa amekuwa akipambana na msongo wa mawazo licha ya kuendelea na harakati zake za kuachia nyimbo kila mara.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Tusimbudde” ameenda mbali zaidi na kudai kwamba amekuwa akiishi kwa hofu kutokana na madeni yanayomuandamana tangu afilisike kiuchumi kipindi cha corona.
“Nina huzuni, hofu na wasiwasi, lakini nitamwambia nani?
Mchezo ni mchezo! Sanaa lazima iundwe. Tumshangilie Mungu daima kwa kujidhirisha kuwa mwenye nguvu na hodari kila wakati.” Ameandika kupitia mitandao yake ya kijamii.
Mashabiki wake na watu mashuhuri wamempongeza kwa kuweka wazi safari yake kupambana na msongo wa mawazo huku wakimtakia afueni ya haraka kutoka kwa hali anayopitia kwa sasa.