Rapa Gravity Omutujju amejibu madai ya Bebe Cool kuwa anapaswa kuoga kila mara ili aweze kufikia kiwango chake cha maisha.
Hii ni baada ya Omutujju kumtaka bosi huyo wa Gagamel kustaafu muziki na kuwapa nafasi vijana wachanga waendeleze gurudumu la kuupeleka muziki wa Uganda kimataifa.
Sasa kupitia mitandao yake ya kijamiii rapa huyo amesema kuwa yeye huwa anazingatia sana masuala ya usafi kwa kuoga kila siku, hivyo Bebe Cool hapaswi kutumia suala hilo kuficha ukweli kwamba anatakiwa kustaafu muziki.
“Tunaoga na kuvaa vizuri, kwa kweli hata tunanukia vizuri. Unaogopa uhalisia na mabadiliko. #kizazi kipya kinatawala duniani kote,” Gravity alichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii.