Rapa Gravity Omutujju amefunguka na kudai kwamba nusura ajiondoe kwenye tamasha lake lijalo kutokana na changamoto za promota wake anayejulikana kama Norbert.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Omutujju amesema Promota huyo amekuwa akihujumu tamasha lake kwa kuamini maneno ya watu kuwa amekuwa akitoa tiketi za bure kwa mashabiki, jambo lililomfanya Nobert kutofanya maandalizi mazuri ya onesho hilo.
Hitmaker huyo wa “Tusimbudde” amesema alilazimika kumrejesha promota huyo baadhi ya pesa za maandalizi ya tamasha lake ambapo amedai kwamba kwa sasa anafanya kazi na promota Balaam Barugahare ambaye aliingilia kati kumsaidia kwani angehairisha onesho lake ingeathiri chapa yake ya muziki,
Tamasha la Gravity linatarajiwa kufanyika Oktoba mosi mwaka wa 2022 huko Cricket Oval, Lugogo.