Juzi kati mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool aliachia wimbo wake mpya uitwao”Gyenvudde” ambao unasimulia mafanikio yake katika tasnia ya muziki. Katika wimbo huo, ameelezea safari yake ya muziki na changamoto ambayo amekutana nayo hadi hapa alipofika.
Mapokezi ya wimbo huo kutoka kwa mashabiki zake yamekuwa mazuri sana kwani wengi wamejitokeza kwenye mitandao yake ya kijamii kumshukuru kusimulia hadithi yake na kusaidia tasnia ya muziki nchini Uganda kukua kwa miaka mingi.
Rapa Gravity Omutujju, hata hivyo, amesema wimbo wa “Gyenvudde” wa mtu mzima Bebe Cool hauna mashiko kwani amesikitishwa na hatua ya bosi huyo wa Gagamel kuachia muziki usio na maudhui mazuri.
Omutujju ameenda mbali zaidi na kuhapa kumpeleka Bebe Cool katika shule ya muziki ili aweze kupewa mafunzo ya uandishi wa nyimbo.
Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa Gravity Omutujju kumshambulia Bebe Cool kwani mwaka mmoja uliopita, hitmaker huyo wa “Bitandise” alimtolea uvivu Bebe Cool na mke wake Zuena.