Rapa Gravity Omutujju amesema msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi anahitaji kusaidia kimawazo kabla ya utundu wake kumuaharibu chapa yake za muziki.
Katika mahojiano yake Omutujju amesema mrembo huyo anahitaji kufunzwa namna atakavyobadili miendo yake ya maisha kama kweli anataka kudumu kwa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.
Kauli yake inakuja kipindi hiki Winnie Nwagi anasuasua kwenye suala la kuwatafuta wafadhili wa onesho lake la muziki ambalo litafanyika mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Inadaiwa kuwa baadhi ya makampuni hayataki kujihusisha na mrembo huyo kutokana na tabia yake mbaya.
Winnie nwagi ni moja kati ya wasanii watundu nchini Uganda ikizingatiwa kuwa amekuwa akihusishwa na kashfa mbali mbali za ukosefu wa nidhamu ikiwemo kuwatusi na kuwapiga mashabiki zake.