You are currently viewing Gravity Omutujju amwaga machozi baada ya familia yake kushambuliwa mtandaoni

Gravity Omutujju amwaga machozi baada ya familia yake kushambuliwa mtandaoni

Rapa Gravity Omutujju amejipata akiangua kilio hadharani kwa kile alichokitaja kuzidiwa na mashambulizi ya walimwengu dhidi ya familia yake kwenye mitandao ya kijamii.

Katika kikao na wanahabari Omutujju amesema kauli yake kuhusu wasanii Bobi Wine, Jose Chameleone na Bebe Cool ilikunuliwa vibaya na mitandao mbali mbali ya burudani nchini Uganda, kitendo ambacho amedai kimewafanya watu kumzushia kila aina matusi kiasi cha kuwaingiza watoto na mke wake kwenye purukushani hiyo.

Hata hivyo hitmaker huyo “Enyama” ambaye amekuwa akijigamba mtandaoni, amelazimika kuomba radhi kwa matamshi yake ya chuki dhidi ya wasanii hao wakongwe kwani huenda ikachafua brand yake ya muziki ambayo ameipambania kwa miaka mingi.

Kwa muda wiki moja sasa Gravity Omutujju amekuwa gumzo mtandaoni alipojaza ukumbi wa Cricket Oval kupitia tamasha lake lakini pia kuhusu kauli tata aliyotoa dhidi ya wasanii Bobi Wine, Jose Chameleone na Bebe Cool ambapo alinukuliwa akiwataka wastaafu muziki na kuwapisha wasanii wapya waendeleza harakati ya kuupeleka muziki wa Uganda kimataifa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke