You are currently viewing GRAVITY OMUTUJJU APINGA HATUA YA SPICE DIANA NA SHEEBAH KUMALIZA UGOMVI WAO

GRAVITY OMUTUJJU APINGA HATUA YA SPICE DIANA NA SHEEBAH KUMALIZA UGOMVI WAO

Rapa kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amepuzilia mbali suala la msanii Spice Diana na Sheebah Karungi kutangaza kumaliza ugomvi wao kwenye listening party ya Stargal EP mwishoni mwa juma lilopita.

Katika mahojiano na Galaxy FM Omutujju amesema wawili hao walitumia jambo hilo kutafuta mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni kwani haamini kama kweli warembo hao walizika tofauti zao kutoka kwa mioyo yao.

Haikushia hapo Hitmaker huyo wa ngoma ya “Big Boys” ameenda mbali zaidi na kumtolea uvivu Spice Diana na meneja wake Roger Lubega kwa kusema kwamba ni wanafiki kwa sababu hawajawahi watakia mema wasanii wengine kwenye shughuli zao za kimuziki.

Hata hivyo amehapa kuanika maovu yote ambayo Spice Diana na Roger Lubega wanafanya nyuma ya pazia hivi karibuni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke